Ijumaa 12 Juni 2026 - 15:48
Ongezeni Utukufu wa Uwepo wa Wananchi na Vijana wa Iran Mitaani, na Imarisheni Zaidi Utamaduni wa Kishujaa na Roho ya Muqawama/ Taifa la Iran Limeandika Ukurasa wa Dhahabu Katika Historia ya Nchi Hii kwa Zaidi ya Siku Mia Moja

Hawza/ Taifa tukufu na lenye heshima la Iran, hususan vijana wapendwa, kwa uwepo wao kwa zaidi ya siku mia moja katika viwanja na maeneo mbalimbali, wameandika ukurasa wa dhahabu katika historia ya nchi hii ambao umekuwa chanzo cha mshangao na taharuki kwa walimwengu. Jambo hili la kipekee lina mchango mkubwa katika kuwakatisha tamaa maadui, na pamoja na kustahiki pongezi na kusifiwa, linapaswa kuendelea hadi mipango ya maadui na vibaraka wao itakapong’olewa kabisa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawzamatini ya ujumbe wa Ayatullah A'rafi, Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّهِ قَرِیبٌ

اَلسَّلامُ عَلَیْکَ یا اَباعَبْدِاللَّهِ وَ عَلَی الاَرْواحِ الَّتی حَلَّتْ بِفِناَّئِکَ

Kuvunja ahadi na kupinga mikataba kumekita mizizi katika tabia na undani wa nafsi za wakubwa wenye kiburi wa Marekani na Wazayuni; إِنَّهُمْ لَا أَیْمَانَ لَهُمْ. Kwa mara nyingine tena, katikati ya usitishaji vita na kubadilishana ujumbe, wameonesha tabia yao ya kishetani, utamaduni wao wa hila, udanganyifu na uvunjaji wa ahadi na mikataba. Hivyo, Lebanon pendwa na kitongoji cha Dhahiya chenye fahari vilishambuliwa na majambazi wa Kizayuni, huku Wamarekani wapenda vita, sambamba na kuendeleza mzingiro wa kidhulma wa baharini, wakikubaliana na mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel mnyakuzi na kuonesha sura yao ya uchochezi wa vita na uvunjaji wa ahadi katika namna yake mbaya zaidi.

Hatua hizi za kishetani, uvunjaji wa ahadi na kukiukwa kwa sheria za kibinadamu na za kimataifa, zimetoa fursa kwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi lenye nguvu, vikosi vya silaha vya Iran vilivyo jasiri, na mkondo wa Muqawama nchini Iran, Lebanon, Yemen, Iraq na sehemu nyingine za mhimili wa Muqawama kusimama kwa nguvu, kuwashushia moto wavamizi wadanganyifu na wasio na huruma, na kuwalazimisha kusalimu amri. Na njia hii itaendelea, Inshaallah.

Hawza na taasisi zake, zikifuata mwenendo wa Marajii wakubwa wa taqlidi na Kiongozi Mkuu (baraka zao zidumu), sambamba na kutoa shukrani na pongezi kwa vyombo vya kijeshi, polisi na usalama, vikosi vya silaha vilivyo imara na jasiri, Basij yenye heshima na matawi mbalimbali ya mhimili wa Muqawama nchini Lebanon na katika eneo lote, vinasisitiza tena mambo yafuatayo:

Zama mpya ya nguvu ya Iran, Uislamu, mhimili wa Muqawama na Umma wa Kiislamu imeanza. Mahesabu na mahusiano ya kidhalimu na ya kikoloni yaliyokuwa yakitawala dunia na eneo hili yameanza kuyumba na kubadilika, dalili za awali za mahusiano na mahesabu mapya yanayozingatia maslahi ya wanyonge wa dunia, Umma wa Kiislamu na taifa la Iran zinaanza kung’aa na kuzaliwa, mgeuko huu mkubwa wa kihistoria na kimkakati unategemea mwamko, ufahamu, mshikamano, kujitolea, kujitoa mhanga na muqawama wa jumla katika nyanja zote za kijeshi, kiuchumi, kijamii na kitamaduni nchini Iran na katika eneo lote.

Taifa la Iran lililo makini, mhimili wa Muqawama, wasomi, wenye fikra pana, mihimili mitatu ya dola, viongozi na taasisi husika, wanapaswa kupanga na kuchukua hatua zinazolingana na mapambano haya makubwa na vita hivi vya hatima, kwa ajili ya kutetea heshima na utukufu wa Iran na Uislamu, Sote, pamoja na wanazuoni wa dini, hawza na vyuo vikuu, tuna jukumu maradufu katika jambo hili.

Pamoja na kupongeza utayari wa vikosi vya silaha vipendwa, tunatumaini kuwa utayari huu na hatua za haraka na sahihi zitaendelea na kuimarishwa zaidi. Kwa mujibu wa maelekezo ya Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Silaha, miundombinu yote muhimu inapaswa kuandaliwa na mipango sahihi kuwekwa, ili kuwabana maadui na kufanya mazingira yawe magumu kwao.

Pia gharama za kuvunja usitishaji vita na kuendeleza hali ya “si vita wala si amani” zinapaswa kuongezwa kwa adui, na fursa ya kujijenga upya na kurejea katika hali ya kabla ya vita inyimwe.

Taifa tukufu na lenye heshima la Iran, hasa vijana wapendwa, kwa uwepo wao kwa zaidi ya siku mia moja usiku katika viwanja na maeneo ya miji na vijiji, wameandika ukurasa wa dhahabu katika historia ya nchi hii ambao umekuwa chanzo cha mshangao na taharuki kwa walimwengu. Jambo hili la kipekee lina mchango mkubwa katika kuwakatisha tamaa maadui, na pamoja na kustahili kupongezwa na kusifiwa, linapaswa kuendelea hadi mipango ya maadui na vibaraka wao itakapong’olewa kabisa.

Kwa kuzingatia hali ya sasa na uvunjaji wa ahadi unaojirudia, haiwezekani kutegemea tu kubadilishana ujumbe na mazungumzo, ni lazima kuchukua hatua kwa busara ya hali ya juu ili kukidhi mahitaji ya wananchi, kuendeleza nchi na kujenga upya uharibifu uliotokea, ni lazima kuchukuliwa hatua zinazolingana na hali ya sasa na mazingira ya vita kwa kuzingatia uchumi wa muqawama, usimamizi wa migogoro na jihadi ya vitendo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha